Share |

Sultan kuwa tayari mapema Feb!

Msanii na mmiliki wa Bendi ya B-Band, Banana Ali Zorro, yuko kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kurelease albam yake mpya mapema mwezi Februari.

Albam hiyo iliyopewa jina la ‘Sultan’ itakuwa na jumla ya nyimbo  nane.

Akiongea na mtandao huu hivi juzi, Banana alisema albam hiyo ilikuwa itoke tangia mwishoni mwa mwaka jana..lakini aliichelewesha ili kukamilisha video ya wimbo 'NUNDA'.

“Hiyo ndio kazi ambayo ninayo kwa sasa na kikubwa nilichokuwa nasubiri ni kumalizika kwa video ya yangu ya wimbo wa ‘Nunda’, ambayo tayari imekamilika hivyo mashabiki wangu wasubiri kuona ujio mwa albam pya,” alimalizia.