Share |

Unataka Dining Room yako iwe vipi?

Dining room ni sehemu ambayo hutumika kulia chakula. Nyumba nyingi huwa na chumba hiki lakini huwa hakitumiki maana watu wamezoea kula chakula kwenye makochi huku wakiangalia televisheni.

Ili watu wa familia yako wafurahie na wapende kula kwenye dining room inakupasa kuwa mbunifu ili pawe ni mahali penye mvuto na kumfanya mtu ajisikie vizuri kula mahali hapo.

Kwanza kabisa dining room yako iwe safi na iliyopangwa vizuri. Hili ni jambo la muhimu sana, sio unaweka vitu vingi kila mahali hadi unapoteza mvuto wa dining room yako.

Pia meza na viti viwe vyenye hali nzuri na vya kuvutia. Weka kitambaa kizuri kwenye meza ya kulia chakula na ikiwezekana uweke na maua ya asili kati kati ya meza ili kuongeza mvuto zaidi.

Wakati wa kuandaa chakula weka table mats za kuvutia pamoja na napkini ili kuleta umaridadi zaidi na kumfanya mlaji kufurahia mlo wake zaidi.

Kama kabati la vyombo lipo dining room hakikisha vyombo vimepangwa vizuri na sio kujaza vyombo bila mpangilio.

Na baada ya kula usafi ufanyike na kuiacha meza na chumba chote katika hali ya usafi. Kuacha vyombo vichafu au kutobadili kitambaa cha meza mara kwa mara kutaondoa hamu ya kuitumia na kusababisha watu kupakua chakula na kwenda kula sebuleni kwenye makochi.
 

Images: