Apollo na nyoka wapigwa stop
Wanaapollo, nyoka na wachimbaji wengine wadogo Mererani wamekumbwa na pigo kali baada ya migodi karibu 30 kufungwa.
Kufungwa kwa migodi hiyo ya madini aina ya Tanzanite ni kutokana na kudaiwa kuwa inaingilia eneo la kampuni mwekezaji ya Tanzanite One.
Kamishna wa Madini, Dk Peter Kifumo alitoka na agizo hilo na wenye migodi hiyo wameshakabidhiwa barua za kutekeleza amri hiyo.
Migodi iliyofungwa ni ya mipakani ya kitalu B inayomilikiwa na wachimbaji wadogo iliyoko karibu na kitalu C kinachomilikiwa na Kampuni ya Tanzanite One.
Hivi sasa uchunguzi unafanyika na maafisa wa kampuni ya madini kubaini kama migogoro hiyo ina ukweli halisi ili kuona uwezekano wa kufungua tena migodi hiyo kutokana na kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa kugombania maeneo ya uchimbaji.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala