Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Saidieni Stars kwa jezi original

Uzi mpya wa vijana wa Taifa Stars unaotamba na watakaokuwa wametinga katika Uwanja wa Kirumba Mwanza umeibuka na fundi fake mitaani.

Fundi huyo wa mitaani alibambwa akisukuma jozi hizo dhaifu kwa kutumia ubunifu halali wa kampuni ya Zizzou Fashion Entertainment iliyopewa tenda ya kuitengeneza na Shirikisho la Mpira wa Miguu -TFF.

Kuibuka kwa jezi hizo kumekuja wakati leo Taifa Stars itakapojirusha katika uwanja wa Kirumba kujaribu kugeuza kibao cha magoli 4 kwa nunge dhidi ya timu ya Senegal.

Msemaji wa kampuni hiyo alisema kampuni yake ilipigiwa pande la kutengeneza jezi hizo ili Watanzania wazinunue katika kuunga mkono timu yao kwa kuwaongezea mapato yatakayowaongezea moyo zaidi wa kucheza na labda kufanikiwa kuibuka na ushindi ambao ndio lengo letu.

Hivi sasa jitihada ya kumfikisha mahakamani mhusika huyo aliyetajwa kwa jina la Fundi (basi) zinafanyika kwani tayari jezi zake zipo kibao mitaani.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.