Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Ilivyo kwa wengine nao ni haki yao

Ridhwani Kikwete, Amina Chifupa, Vailet Mzindakaya, ni baadhi tu ya majina ya watoto wa vigogo wanaogombea nafasi za kugombea ujumbe wa NEC na nafasi nyingine za uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Akitetea uamuzi huo Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alisema ameshangazwa na baadhi ya watu kulalamikia kitendo hicho kwani ni haki ya kila mmoja kugombea uongozi.

CCM ndio chama pekee wanachokijua tangu utotoni kwao na baba zao ni viongozi kwa hiyo wanafuata nyayo za wazazi wao, alisema Makamba na kuongeza kuwa hakuna baya kwa watoto hao kugombea uongozi.

Baadhi ya Wabongo wamekuwa na maoni tofauti juu ya watoto hao kugombea nafasi za juu ndani ya CCM huku wengine wakiunga mkono kitendo hicho na wengine wakikandia hali hiyo kuwa ni sawa na kupeana madaraka.

Lakini ni mara nyingi, sehemu nyingi na hata nchi nyingine watoto wamekuwa wanakuwa viongozi baada ya baba zao kutawala kama ilivyo kwa Rais G. Bush wa Marekani anayetawala baada ya baba yake Bush kuitawala Marekani.

Makamba alisema kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya CCM ili mradi ana sifa na kutimiza masharti yanayotakiwa



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.