Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Kuweni makini idadi ya watoto

Wabongo wameshauriwa kuwa makini kwa idadi ya watoto wanaozaa ili kuendana na uwezo wa kuwalea kwani hivi sasa ongezeko la watoto katika familia ni limepanda hadi kufikia asilimia 6.3.

Chama cha Madaktari wa magonjwa ya akina mama kimetoa tahadhari hiyo na kuongeza kuwa makisio yanaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2025 idadi ya Wabongo itakuwa imeongezeka kwa asilimia 60 na kufikia mil. 53.

Prof Richard Lema aliwashauri Wabongo kupunguza kasi ya ongezeko la watu ili liendane na ukuaji wa uchumi wa kifamilia ili kukidhi mahitaji ya kijamii ikilinganishwa na mwaka 1978 idadi wa watu ilipokuwa milioni 15.

Kutokana na wingi wa wanafamilia wengi wameshindwa kumudu gharama za maisha na hivyo kujiongezea umaskini wa kifamilia na wa Taifa zima.

Mabingwa hao waliongeza kuwa kwa kupunguza idadi ya watoto katika familia itasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto na kwa uwezo wa familia kuwatunza vizuri..



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.