Wanaume wabakaji wakomeshwe vilivyo
Imeibuka katika pita pita na kupendekezwa kuwa wanaopatikana na makosa ya kubaka wanawake na watoto wafanyiziwe kama ile midume ya ngombe na mbuzi.
Kuhasiwa ndio adhabu mpya waliyopendekeza ili kipengele cha sheria ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 irekebishwe kuendana na ukubwa wa kosa lenyewe.
Sheria hiyo itawatia hofu wabakaji na hivyo kutokomeza vitendo hivyo vinavyozidi kuongezeka nchini.
Mapendekezo hayo yalitolewa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania -TAMWA wanaojadili namna ya kupunguza kuolewa kwa watoto wadogo wa kike.
Walitaka pamoja na hayo kipengele kinachoruhusu mtoto wa kike wa umri wa miaka 14 au 15 kiondolewe kwani kinamkandamiza mtoto wa kike na hasa katika umri huu wa kwenda shule.
Msichana wa miaka 14 huruhusiwa kuolewa kwa amri ya Mahakama wakati wa miaka 15 hufanya hivyo kwa ruhusa ya wazazi wake. Kwa mtaji huu kuna mapendo hapa???!!

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala