Email moja kwa moja Polisi
Polisi mkoani Mbeya imeibuka na bonge la wazo kupokea maoni, taarifa chochote kuhusiana na uhalifu kwa njia ya tovuti.
Tovuti hiyo; rpcmbeyainformation@yahoo.com itakuwa inapokea maoni ya na taarifa za uhalifu ili kwenda sambamba na simu za mkononi zilizofagiliwa sana kwa kuwaweka kati wahalifu.
Kamanda wa Polisi Mbeya Suleiman Kova alisema wameibuka na tovuti hiyo kwenda sambamba na teknolojia ya habari ili kufanikisha upatikanaji wa habari kutoka sehemu yoyote na kwa gharama nafuu zaidi.
Alitaja sehemu wanazotarajia kupata habari kuwa ni kutoka nchi jirani za Malawi, Zambia na mikoa mingine ya jirani inayopakana na Mbeya.
Taarifa hizo zitakuwa za siri na watoa taarifa watakuwa wanapatiwa maendeleo ya taarifa walizotoa kulingana na uchunguzi utakavyokuwa unaendelea.
Kuibuka kwa matumizi ya kompyuta kuwasiliana na jeshi la Polisi ni hatua mpya sambamba na aliyoanza Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema ya kutumia vilonga mbali kwa kuanika wazi namba za simu za Maafisa wa juu wa jeshi hilo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala