Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
TAMWA waongopea wengine?

Wanawake wenyewe kwa midomo yao wamepinga kauli ya akina mama wa TAMWA eti kwamba wanawake wanaoishi katika ndoa wanaishi maisha ya kitumwa.

Huku wakiringia mahusiano yao na waume zao, wamedai kuwa TAMWA imechukulia tatizo la mtu mmoja au baadhi ya akina mama kuwa ndio matatizo ya ya wanawake wote wakati si kweli.

Mmoja wa akina mama hao Margareth Mtweve (mwanasheria) alisema ameshangazwa na kauli ya Mkurugenzi wa TAMWA Bi Ananilea Nkya na ana wasiwasi endapo ameolewa, ameachika au ana uzoefu gani wa masuala haya.

Walitakiwa kufanya uchunguzi kwanza kwani wamekuwa wakishabikia makosa ya akina baba zaidi wakati kuna akina mama wanaotelekeza watoto wao na wengine wanaonyanyasa waume zao.

Wengine waliolalamikia kauli hiyo ni Beatrice Kolimba na Salome Daya waliosema kuwa kauli hiyo imewashushia heshima kwani waliolewa wote wataonekana kama ni watumwa mbele ya jamii wakati wengi hufurahia ndoa zao na wenza wao.

Kauli kama hizo zinaweza kuibua matatizo kwa walio katika ndoa na hata wasichana na kuwafanya kuwaogopa wanaume na hata masuala ya ndoa na kuwafanya waishi maisha nje ya ndoa na hivyo kuongeza kasi ya maambukizi ya ukimwi.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.