Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Tujiandae kuchumpa kwa umeme?

Tujiandae kwa bei kubwa zaidi pindi sasa TANESCO wamebaniwa mshiko wa kujiendesha kutoka serikalini wa sh. bilioni 10/-.

Wenyewe wametamba kuwa kazi zitaendelea kama kawa, lakini usemi huu una walakini ndani yake kwani ni karibuni tu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dr Idris Rashid alikuwa analalamikia hali mbaya ya kifedha.

Alisikika akisema kuwa ukata unalielemea shirika lake na linashindwa kukarabati miundombinu yake mingi iliyozeeka nchini kote.

Mshiko uliokuwa unatolewa na serikali ni kuipiga tafu TANESCO katika kulipa deni la IPTL (dola za Marekani mil. 2.8), Songas (dola mil.6.0) na nyingine kununua umeme pale inapohitajika kufanya hivyo.

Hivi sasa shirika hilo limesema litaanza kujiendesha kibiashara na kukopa fedha za kujiendesha kutoka benki lakini kimbembe chake ni kwa wateja wao.

Dk Rashid aliongeza kuwa msumari utashindiliwa kuhakikisha wateja wote wanalipa bili zao kwa wakati ili kuliwezesha shirika hilo kujiendesha.

Hata hivyo malalamiko ya muda mrefu ya TANESCO ni dhidi ya serikali kwani ndio wadaiwa wakubwa wa bili za umeme.

Au tuseme serikali inataka kumalizana nao kwa ruzuku waliokuwa wanawapatia?



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.