Uandikishaji sasa ni bomba zaidi
Usumbufu wa kufunga safari hadi mikoani na Wilayani kuandikisha masuala yote ya uzazi, vifo na ndoa yamepitwa na wakati kwani huduma hiyo imesogezwa katika Kata.
Kwa mtaji huo wananchi wengi watakaokoa walau visenti vyao na kujiokoa na safari ndefu za kuibukia Wilayani na Mikoani kusaka huduma hiyo muhimu, na wakati mwingine ukutane na -Njoo Kesho.
Kutokana na usumbufu huo na hali mbaya ya kiuchumi katika kufuatilia vyeti hivyo serikali imeamua kusogeza huduma hiyo karibu zaidi ili kupata takwimu sahihi za matukio hayo.
Awali wengi walikuwa wanakacha kuandikisha matukio hayo na hasa ya vifo na uzazi na hivyo kutoa takwimu isiyo sahihi serikalini juu ya idadi kamili ya matukio hayo na kupindisha mipango muhimu ya maendeleo.
Akifafanua uamuzi huo Mkuu wa Wilaya (Dodoma Mjini) John Tupa alisema vilevile uamuzi huo umefikiwa ili kukwepa uwepo wa vyeti vingi fake vinavyosambaa sehemu kama kuomba pasi za kusafiria, kujiandikisha shuleni na kwingineko.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala