Vikojozi wa viambaza kati
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wanaojiachia na mkojo hovyo katika sehemu za wazi wametahadharishwa kwani sheria za kukabiliana nao inasukwa vizuri zaidi.
Agizo hilo lina nia ya kutokomeza harufu mbaya inayoibuka katika kona na vichochoro vya jiji hilo kutoka kwa wachafuzi wasio na aibu na kuunguzwa kwa mimea katika kona hizo.
Akisisitiza kubebwa mzobemzobe kwa vikojozi hao, Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Samuel Kamote aliitaka Halmashauri wa jiji hilo kulinda hadhi ya usafi na kutunza mazingira kwa kufuatilia kwa makini sheria zilizopo.
Jiji la Mwanza limepanga mkakati huo ikiwa ni hatua ya kuendelea kutesa kutokana na usafi na mandhari ya kuvutia baada ya kutangazwa kuwa jiji safi nchini ikiwa ni mara ya pili mfululizo kupata ujiko wa tuzo hiyo.
Jiji Dar faini ya kuwabana vikojizi ovyo mitaani ni sh. 20,000/- za papo hapo lakini nina mashaka kama inafanya kazi kutokana na vituo kibao vya daladala kuwa na vikona vyenye harufu kali na majani yaliyokaukaaaaa.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala