Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Traffic Police atiwa kibano kweupee

Isije kuwa zile za akina Mungiki wa Kenya zimetinga Bongo, kwani baadhi ya wenye michuma, makonda na abiria wamemzonga mwanausalama aliyekuwa zamu ya kuongoza magari na kuanza kumsulubu.

Kisa hicho kiliibuka Magomeni traffic lights wakati askari huyo alipozuka ghafla katikati ya taa zilizokuwa zinafanya kazi na magari kupita, na kuanza kuongoza magari kwa kupunga mkono.

Mida hiyo ikiwa ni saa sita mchana, Askari huyo wa usalama barabarani aliendelea kuruhusu magari ya pande zote kwa zamu isipokuwa yale yaliyokuwa yanatokea katikati ya jiji kwa maana ya Posta, Kariakoo na kwingineko.

Magari hayo yakaendelea kupita hivyo kwa zamu huku foleni ya kutoka town ikizidi kuwa ndefu na dakika zinaendelea kuyoyoma. Ghafla nusu saa na mara saa moja magari ya mjini yapo tu.

Ta-ra-ti-bu baadhi ya madereva, makonda na abiria waliokuwa mbele ya foleni wakaanza kumsogelea askari huyo kuulizia iweje anasahau kuwaruhusu.

Askari huyo akawapandishia kuwa wasimfundishe kazi, kwanza warejee kwenye magari yao na waendelee kusubiri.

Kitendo hicho kiliwaudhi na wakaanza kumzonga huku baadhi yao wakiruhusu magari ya upande wao kupita. Hali hiyo iliyakusanya magari mengi kwenye makutano hayo na mwishoni yakashindwa kuendelea kupita.

Wale waliomzonga askari walianza kumshambulia kwa kibano na askari wa watu ghafla akalambwa mtama na mara akajikuta chini.

Askari huyo aliokolewa na askari wenzake waliozuka eneo hilo wakiwa ndani ya Defender na kupiga risasi za rasharasha hewani, kisha kumwokoa mwenzao na kumsomba mmoja wa waliotoa kibano hicho na kuishia kwa kasi kuelekea kituo cha Polisi Magomeni.

Kamanda wa Polisi Kinondoni alipoulizwa juu ya hilo alisema, taarifa hiyo haijafika kwake ila akaongeza kuwa kuzuiwa kwa magari hayo kulitokana na uwepo wa msafara wa kigogo mmoja serikalini aliyekuwa anakatiza mitaa hiyo.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.