Kuanikwa mshiko wa MP's noma
Kufichuka kwa posho na marupurupu kibao ya Wabunge kabla ya kupitishwa kwa muswada wake Bungeni umechangia wanusa nusa na mapaparazzi kupigwa mkwara wa no entry katika kamati za Bunge.
Pamoja na kutokuwepo kwa maelezo ya wazi kutoka kwa Katibu wa Bunge Damian Foka, kuna taarifa kuwa timu nzima wa Waheshimiwa hao wamechukizwa na kitendo cha vyombo vya habari kuanika ongezeko la mishiko yao inayotarajiwa kusomwa Bungeni katika kikao kijacho.
Wamechukizwa na kitendo cha fedha zao kuwekwa hadharani, badala ya kuwa siri na hivyo kuhofia wananchi wao kuwachomoa uchache kwani wanajua wanajua wanachovuna.
Baadhi ya wananchi wamechukuliwa uamuzi huo wa Wabunge kama ni kaubinafsi fulani kwani yanapokuja masuala ya maendeleo hupigia debe kibao na kuvitaka vyombo vya habari kulipigia debe la nguvu.
Kwa habari zaidi juu ya mshiko huo wa Wabunge soma habari ya -Wabunge nao kulamba mshiko zaidi- ndani ya Dhw

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala