Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
'Endesha gari kontena hilo'

Masuka na makonda wa safari daladala jijini Dar na hasa vipanya wamenyooshewa kidole cha ole kutokana na tabia yao ya kuwanyayapaa abiria walioshiba yaani wanene.

Hali hiyo inatokana na viti vidogo vilivyobanana vilivyo ndani ya magari hayo visivyowezesha watu wanene haswa kuenea vizuri.

Pale inapobidi abiria wa aina hiyo kukalia viti hivyo, basi hukaa kwa idadi pungufu yaani watatu badala ya ile ya kawaida ya watu wanne.

Hali hiyo imekuwa inawakera makonda na masuka kwani wanahesabu kuwa watu wanene wanawasababishia hasara kwa kusafirisha vichwa (kama wanavyoita abiria) vichache zaidi kuliko wanavyotaka.

Pale wanene wanapojichanganya na abiria wengine inashindikana kuwanyanyapa moja kwa moja. Lakini kwa mtindo wa Dar wa kupakia juu kwa juu yaani bila kuzingatia vituo, inapokuwa ni mtu mnene anataka kupanda daladala -yanapita kwa kasi kama vile hawajamwona huku wakiwaita jina la utani la kontena.

Suka endesha gari achana na kontena hilo, ndiyo maneno yanayosikika pindi wanapowaona abiria kama hao.

Hali hubadilika pale wanapomwona mtu mwingine wa kawaida hata kama anapita zake barabarani basi hupigiwa honi kibao huku akiulizwa -vipi unakwenda?-.

Tayari taarifa zimeshawasilishwa kwa wasimamizi wa usafiri nchi kavu na majini SUMATRA ili kukomesha tabia hiyo.

Na bila kupinga huu nao ni unyanyapaa dhidi ya watu wenye maumbile makubwa aka wanene.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.