Haitoshi na bado tunagawa hovyo
Hebu piga hesabu mshiko unaotolewa kama mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ulivyo kiduchu, unavyobaniwa na sasa unapigwa panga hata na madenti wa nje.
Maandamano na migomo ya wanafunzi wa elimu ya juu hayaishi kwa kudai kulipiwa asilimia 100 ya ada ya vyuo, na kama kawa serikali via Bodi ya Mikopo wanadai hakuna fedha zaidi.
Kumbe kuna madai ya madenti wa nchi za nje nao wanakopeshwa fedha halali kwa madenti halali wa Kibongo tu.
Habari hizo zinazoendelea kuchunguzwa zinasema kuwa kuna madenti 11 raia wa nchi za nje, wanaosoma Chuo Kikuu Mlimani waliojaza fomu na kupata mikopo ya ada ya elimu ya juu.
Hatutaki kuhisi kilichotokea kwani masharti ya kupata mikopo hiyo ni mengi ikiwa ni pamoja na kuthibitisha kuwa mwombaji ni raia wa Bongo. Nini kilitokea hatujui -labda baada ya uchunguzi.
Hayo yanatokea huku madenti wengine 29 wakiwa wamekwama nchini Ukraine (Ubalozi wa Uingereza) kwa kushindwa kulipia ada ya masomo katika vyuo walivyokuwa wanasoma.
Serikali nayo imenawa mikono kwanza kwa kuwa haina fedha za kuwalipia na kwamba wanafunzi hao walikwenda huko kwa udhamini binafsi.
Kimbembe cha wageni hao waliolamba Bingo yetu bado kinachunguzwa na taarifa itatolewa yote yakikamilika. Hivyo ndivyo walivyosema.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala