Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Tukae mkao gani -wa kilio?

Tumeshazoea mara vikao vya Bunge vinapokaa badala ya kutoka na majibu ya kero kibao zinazotukabili tunaanza kujiandaa kuumia aidha kwa bei ya vitu kupanda, ushuru na kodi ya pale kuongezwa.

Kero za barabara mbovu, foleni ndefu jijini Dar, hospitali zisizo na dawa na wagonjwa kulala chini, wakulima wachovu ndio majibu tunayotarajia yatafutiwa ufumbuzi mara Wabunge wetu wanapotinga Dodoma.

Achilia mbali mshiko wanaolamba (mwanangu unatisha) lakini usingeonekana kubwa hivyo ukichanganyia na mashangingi kama wangekuwa wanachakarika vilivyo japo basi kupunguza mizigo mizito ya ukapera unaowakondesha Wabongo.

Kwa hiyo ile raha ya kusikilizia Bungeni walau tutapungua kwa hili na lile kupata ufumbuzi, tunakaa mkao wa kujiandaa kupanda kwa aidha ushuru wa mgari, kodi ya ushuru wa thamani wa bidhaa tunazotarajia, kupitishwa kwa miswada ya kuzidi kutubana na of course bila kusahau nyongeza ya posho na mishahara ya Waheshimiwa wapendwa Wabunge wetu.

Na kama vile waliokwisha kujulia hali hii, wafanyabiashara mitaani hudunduliza baadhi ya bidhaa muhimu wakitarajia kuzipandisha bei kwa kujua kuwa Wabunge watapandisha kodi zake na hivyo kujipatia faida zaidi.

Ingekuwa bomba mbaya endapo kila wakati kama huu wa vikao vya Bunge tukae mkao wa kula tukitarajia kero zetu hatimaye zimepata mkombozi na zimefika jikoni kupatiwa suluhisho.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.