Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Kampuni ya biashara CCM

Bonge la mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Dar kwenda Mwanza na Kigoma lina pande la Chama cha Mapinduzi ndani yake.

CCM inayolamba ruzuku ya karibu sh. bilioni moja kila mwezi kutokana na kuwa na vigogo wengi wanaotawala imejipachika katika biashara hiyo kama njia ya kujiongezea mapato kupitia kampuni yake ya Tanzania Green Ltd.

Awali CCM pamoja na Waziri Mkuu wa zamani Joseph Warioba walihusishwa na deal lingine la kibiashara la kampuni ya kusafisha dhahabu na kulamba bonge la mshiko kutoka Benki Kuu ya TZ.

Mradi huo ni wa ujenzi wa bomba hilo na kusafirisha mafuta ulioanza miaka 10 iliyopita na sasa umetolewa kwa wawekezaji wa Qatar Oil, Noor Oil na Industrial Technology Ltd ambayo pia ina ubia na Roneg AG ya Ujerumani na Stroytransgaz na Promoteurs ya Urusi na CCM ndani yake.

Awali kampuni ya Africommerce International, Elisante Muro alilalamikia pande hilo akidai mradi huo ulikuwa wao na wamepigwa changa la macho na kunyanganywa mradi huo.

Mradi mwingine kampuni hii iliyohusishwa nao ni mauzo ya asilimia 49 za hisa za Benki ya NMB.

Hakuna lolote lililoibuka juu ya uhalali wa CCM kujiingiza katika biashara za kibongo na huenda hii ni motisha kwa akina Mzee wa Kiraracha Mrema kujikita na chama chako katika mapande ya kibiashara.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.