Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Tutaringa wote tukishapima

Mpango wa Rais JK kushinikiza Wabongo wooooteee kujitokeza kupima afya zao kwa maana ya kama wana virusi vya ukimwi huenda isifanikiwe.

Tahadhari hiyo ni kwa mujibu wa Asasi za kukabiliana na ugonjwa huo kutokana na uhaba mkubwa wa vifaa na urasimu ndani ya Wizara ya Afya.

Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoshuhulikia afya, ukimwi na jinsia, wamesema kuwa kuna upungufu mkubwa wa vifaa vinavyotumika kutoa huduma ya vipimo jna wakati mwingine huchukua muda mrefu kupatikana.

Mratibu wa Muungano huo, Dk Peter Bujari alisema kuwa upungufu wa vifaa hivyo umejidhihirisha pamoja na kwamba hadi sasa ni asilimia 15 tu ya Wabongo waliojitokeza kupima afya zao dhidi ya VVU kulingana na utafiti wa mwaka 2004.

Pamoja na kwamba ushauri nasaha unahitajika kabla na baada ya kupima ikiwa ni pamoja na kutoa huduma muhimu kwa wenye VVU, kuna haja kubwa ya kubadilisha mfumo wa upatikanaji vifaa unaofanyika sasa katika Wizara ya Afya, alisema.

Hivi karibuni katika maelezo yake kwa Waandishi wa Habari, Rais JK aliwataka wananchi wote kujitokeza kupimwa afya zao ili kupanga namna ya kuishi na kuenenda kwa maisha marefu zaidi.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.