Kupatiwa damu ni bure tena bure
Damu inayotolewa kwa wagonjwa kutoka vituo vya afya, zahanati na hospitali ni bure na endapo utadaiwa chochote basi mara moja longa na vibosile Wizara ya Afya au vyombo vya dola kwa hatua za kisheria.
Hayo yamefafanuliwa rasmi na Waziri wa Afya Prof. David Mwakyusa aliyekandamiza kuwa atakayebainika akipokea chochote kidogo kutokana na kumpatia mgonjwa damu atashughulikiwa vilivyo.
Prof. Mwakyusa alisema kuwa damu hiyo hutolewa bure kwani hata vituo hivyo vya afya huipata bure kutoka vituo vinne vilivyopo vya damu salama.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala