Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Wenye ndoto changamkieni tenda

Wabongo wametakiwa kujitokeza na mabizness ideas yatakayowezesha kujipatia mikopo ya kujiendeleza na kufuta umaskini.

Unachotakiwa kufanya ni kuibuka na mradi wako aidha mpya au wa namna ya kuendeleza uliopo katika mpango wa ushindani wa kibiashara -Tanzania Business Plan Competition.

Mpango huo umepewa kauli mbiu ya kimombo ya Believe, Begin, Become na uko chini ya Google.org ya Marekani, Techno Serve na M&M Communications.

Akizindua mpango huo Rais JK alisema kuwa wengi wenye ndoto zao zinazoweza kugeuzwa kuwa kweli endapo wangepatiwa mitaji, teknolojia na namna ya kusimamia miradi yao.

Aliwataka wengi kujitokeza kuchangamkia tenda hiyo katika kufuta umaskini kwa kupata ujuzi zaidi

kuboresha huduma na kupiga mzigo kwa nguvu katika kuhimili ushindani wa kibiashara.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.