Wembe ni ule ule-Maximo
Marcio Maximo ambaye ndiye Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ( Taifa Stars), kwani ameshaanza ziara yake leo ya kwenda mikoani kwa ajili ya kusaka vipaji vya vijana na kuviendeleza.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) Frederick Mwakalebela alisema, kuwa katika ziara hiyo Maximo ataambatana na kocha wa vijana Marcus Tinoco na yeye mwenyewe Katibu.
Mwakalebela alisema ziara hiyo itaanzia Mkoani Morogoro leo na kesho, Jumapili na Jumatatu tutaibukia Iringa, Jumanne na Jumatano tutakuwa tena ndani ya mkoani Mbeya kisha tutarejea nyumbani ndani ya jiji la Kandoro.
Alisema baada ya wiki moja, atakwenda Zanziabar kwa ajili ya ziara ya siku tatu, na mwisho atahitimisha ziara hiyo Lindi pamoja na Mtwara.
Kwani mwezi wa nne kutakuwa na Semina ya Makocha, ambao timu zao zitashiriki ligi kuu inayoendelea hivi sasa nchini.
Kocha huyo ameanza ziara hiyo baada ya kuvunjwa kwa kambi ya Stars, ambapo waliingia kambini kwa ajili ya mechi ya kirafiki na Malawi lakini mechi hiyo iliahirishwa baada ya malawi kushindwa kuja.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala