Yanga kupepea ndani ya Madagascar leo
Msafara wa wachezaji wa kikosi cha Yanga pamoja na viongozi wake, unatarajiwa kutimka leo mchana kuelekea mjini Antananarivo, Madagascar.
Kikosi hicho kitaelekea katika mji huo wa Yanga yaenda Madagascar leo, kwa madhumuni ya mechi ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Yanga inaondoka nchini ikiwa ni siku nne kabla ya mechi hiyo itakayopigwa Februari 17 na mechi ya marudiano itachezwa jijini Dar es Salaam, wiki mbili baadaye.
Katibu Mwenezi wa Yanga Francis Lucas, alisema kwamba msafara wa timu hiyo utaondoka leo saa 8 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
Lucas alisema hadi kufikia jana jioni, benchi la ufundi lilikuwa bado halijafanya uteuzi wa mwisho wa kikosi kitakachoondoka na kudai kwamba kitajulikana muda mfupi kabla ya kuondoka.
Yanga iliyo chini ya Kocha Mserbia Dusan Kondic akisaidiwa na Spaso Sokolovski, inarejea katika michuano ya kimataifa huku ikikumbuka kung’olewa na Esperance ya Tunisia katika Kombe la Shirikisho.
Yanga iliangukia katika Kombe la Shirikisho baada ya kung’olewa katika raundi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini hata hivyo ikafungwa na kutupwa nje ikiwa chini ya Mserbia, Sredejovic Milutin Micho.
Wakali hao walioutema kwa Simba ubingwa wa bara Julai 8 mwaka jana, safari hii wanaingia katika kampeni wakiwa chini ya kocha mwingine na nyota kadhaa wapya.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala