Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Gofu ya vijana kupigwa tarehe

Michuano ya kwanza ya mchezo wa gofu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 19, ilipangwa kusheheni mwishoni mwa wiki hii ndani ya viwanja vya klabu ya Gymkhana Dar es Salaam lakini imesogezwa mbele kwa muda usiojulikana.



Naye Katibu wa Mashindano wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Mohammed Sadiki hakuwa nyuma bali alikuwa na haya ya kusema, kwamba michuano hiyo ya siku mbili iliyopangwa kuanza Februari 16 hadi 17 ya viwanja 36 haitofanyika kama ilivyopangwa awali.

Sadiki alisema sababu ya kuahirishwa kwa michuano hiyo ni kutokamilika kwa maandalizi ya mashindano hayo.

Alisema bado hawajakamilisha maandalizi hivyo wameamua kusogeza mbele siku pamoja na tarehe, kwani itatangazwa hapo baadaye.

Michuano hiyo ni ya kwanza katika historia ambayo ilikuwa ya pili katika kalenda ya mwaka 2008 ya TG iliyotolewa hivi karibuni, kwani ilipangwa kuwa ya wazi kwa vijana wa umri huo ikiwa na lengo la kuvumbua vipaji.

Katibu huyo aliendelea kusema kwamba michuano ya TPC Open iliyopangwa kufanyika kuanzia Machi 8 hadi 9 kwenye viwanja vya Klabu ya TPC Moshi nayo imesogezwa mbele.

Alisema michuano hiyo ya kila mwaka sasa imepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya Aprili na kwa upande wa michuano ya TPC imesogezwa mbele kutokana na ombi la wadhamini wa klabu ambao watakuwa na mashindano ya ndani tarehe hizo.

Katibu huyo alimalizia kwa kusema kwamba Kutokana na kutambua mchango wao na haki ya klabu TGU, klabu hiyo imekubali kusogeza mbele michuano hiyo Kutokana na kuahirishwa kwa michuano hiyo Coast Open iliyopangwa kufanyika Machi 22 hadi 23 kwenye viwanja vya Klabu ya Gymkhana vilivyopo hapa jijini kwani vitakuwa ni vyapili kufanyika mwaka huu.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.