Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Kutoroka kwa wachezaji siyo tatizo-Madega

Huku timu hiyo ikiwa mkoani Dodoma ikiendelea na kambi Kocha Mkuu wa timu ya Yanga, Mserbia Dusan Kondic alisema kwamba lolote linaweza kutokea katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) dhidi ya AS Adema ya Madagaska.



Kondic alisema hicho kitakachoweza kutokea ni kutokana na wachezaji kushuka kiwango, kwa uzembe ao wenyewe wanaoufanya wa kutoroka kambi na kwenda katika starehe.

Kikosi hicho chenye wachezaji 21 pamona na viongozi 8 kiliweza kuondoka jana kuelekea Madagaska kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini, kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika keshokutwa.

Kondic alisema wachezaji wake walicheza chini ya kiwango katika mchezo dhidi ya Polisi Morogoro Jumatatu, na hiyo ilitokana na baadhi yao kutoroka kambini baada ya mchezo na Polisi Dodoma mkoani humo wiki iliyopita.

Alisema amekerwa sana na kitendo hicho ambacho kilifanya wacheze chini ya kiwango katika mchezo na Polisi Morogoro licha ya kushinda mabao 3-0.

Alisema kutokana na hali hiyo hana matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya AS Adema, lakini lolote linaweza kutokea kwani mpira ni dakika 90 na kwamba tayari amewasilisha suala hilo kwa uongozi.

Naye Mwenyekiti wa Yanga Imani Madega ambaye ndiye mkuu wa msafara huo, alisema kutoroka kwa wachezaji sio tatizo kwani kufanya vizuri kwa timu kunatokana na maandalizi na wanaamini wamefanya maandalizi ya kutosha na hivyo wanajiamini kufanya vizuri.

Naye nahodha wa timu hiyo Fred Mbuna alisema mchezo utakuwa mgumu, lakini wamejiandaa vya kutosha na wanatarajia kufanya vizuri.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.