Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Twiga kukomalia mechi za kirafiki

Hatimaye yale maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Stars, kwa sasa yanaendelea vizuri kwa mujibu wa Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa.



Kocha huyo alisema timu hiyo inaendelea vizuri katika programu ya mazoezi, ingawa hakusita kuweka bayana kuwa angefurahi kama ingepata mpambano wa kujipima nguvu kabla ya kuwakabili Cameroon, Februari 23.

Alisema angefurahi kama angepata mechi hata moja kabla ya kuikabili timu hiyo ya Cameroon, itakayo itakayojibweteka ndani ya Uwanja wa hapa nyumbani Februari 23 mwaka huu.

Mkwasa alisema tatizo walilonalo sasa hivi ni kuhusu mechi za majaribio, kwani liko nje ya uwezo wake kwani wenye jukumu hilo ni TFF.

Twiga Stars ingecheza na Afrika Kusini, Zimbabwe katika mechi za kujipima nguvu, lakini ilishindikana kwa kile kilichoelezwa kugongana kwa ratiba.

Naye Daktari wa timu hiyo Sufiani Juma alisema kuwa mpaka sasa majeruhi ni watatu tu, nambao ni Hellen Peter, Rose Chipa na Fatma Bushiri.

Twiga Stars, itashuka dimbani, Februari 23 kucheza na Cameroon katika mechi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.