Sijaridhika na kiwango chenu-Maximo
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars' Marcio Maximo awaonya wachezaji wa timu hiyo ya taifa, baada ya kutoridhika na kiwango walichonacho na kuwataka kuendeleza kiwango chao wanapocheza katika.
Maximo alisema kwamba haridhishwi na kiwango cha baadhi ya wachezaji wa Taifa Star, wanapochezea klabu zao kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.
Alisema ameshuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Simba na Awassa City ya Ethiopia uliofanyika siku ya Jumapili (juzi).
Kocha huyo alisema anachoweza kusema ni kwamba baadhi ya wachezaji wameweza kumkatisha tamaa, kwani wameshindwa kuonyesha kiwango chao na kuonyesha kuwa wanastahili kuwa kwenye timu ya taifa.
Alisema siku zote anapothamini mchezo haangalii kiwango cha timu, bali huangalia kiwango cha mchezaji mmoja mmoja na ubora wake.
Hata hivyo kocha huyo hakusita kuwamwagia sifa wachezaji ambao wameonyesha juhudi na kiwango kilichoonyeshwa na baadhi ya wachezaji, ambao walishawahi kuwa kwenye timu ya taifa na kutemwa kwa sababu ya mbalimbali.
Aidha, Maximo alisema anatarajia kutangaza kikosi cha Stars Machi 15, tayari kwa mchezo wa kirafiki utakaofanyika Machi 26 kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.
Alimalizia kwa kusema Stars inatarajia kwenda Brazil mwanzoni mwa Mei kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya kujiandaa na michezo ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, na ikiwa huko itacheza michezo sita ya kujipima nguvu.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala