Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Shamsi kuwa mgeni rasmi

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) Boniface Wambura, amealikwa katika kutoa tuzo kwa mwanamichezo bora Februari 22 kwenye Ukumbi wa Landmark uliopo hapa jijini.



Naye Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kumtangaza mwanamichezo bora wa mwaka 2007.

Wambura alisema katika hafla hiyo pia itasheheni burudani ya muziki kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Kalunde, inayoongozwa na Deogratius Mwanambilimbi ‘Mzee wa Goba’.

Kwani Wanamichezo watakaowania tuzo hiyo ni wale ambao walifanikiwa kushinda tuzo za miezi kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana.

Wanamichezo hao walioshinda ni pamoja na Haruna Moshi (Januari-Soka), Masoud Amour (Februari-Judo), Josephine Deemay (Machi –Riadha), Ally Mustapha ‘Barthez’ (Aprili-Soka), na Banuelia Brighton (Mei–Riadha).

Wakifuatiwa na Erasto Nyoni (Juni–Soka), Martin Sulle (Julai–Riadha), Kudra Omari (Agosti-Soka), Oswald Morris (Septemba-Soka), Mary Meshack (Oktoba-Kikapu), Japhet Kaseba (Novemba-Kickboxing) na Asha Rashid ‘Mwalala’ (Desemba-Soka).

Wanamichezo bora wa mwezi watazawadiwa cheti, kombe na fedha taslimu sh 200,000 kila mmoja, wakati atakayeibuka mwanamichezo bora wa mwaka, atazawadiwa sh 500,000 na hii itamfanya aibuke na jumla ya kitita cha sh 700,000.

Mwanamichezo bora anayemaliza muda wake ni mwanariadha Samson Ramadhani, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za marathoni kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka juzi, Melbourne, Australia.kuwa





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.