Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Twiga yawatwanga IPP mabao 2-1

Hatimaye timu ya soka ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars, mnamo majuzi ilionyesha uwezo wake wa juu na matumaini ya kufanya vizuri dhidi ya Cameroon, baada ya kuliza IPP kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Karume hapa hapa nyumbani.

Timu hiyo ya Twiga iliweza kuibuka kidedea na ushindi baada ya kujitwalia mabao katika kila kipind, huku ikionyesha soka ya kuvutia katika vipindi vyote viwili.

Bao la kwanza la Twiga lilifweza kuingizwa langoni moja kwa moja na Mwapewa Mtumwa ndani ya dakika ya 2, baada ya bao hilo hawakuzubaa kwani waliendelea kuonyesha soka ya kuvutia na kufanya watu wengi kuwashangilia kwa nguvu.

Ndani ya kupindi cha pili damu ikiendelea kuchemka wana dada haowalipachika tena bao lingine la pili wavuni, lakini mwamuzi Othman Kazi alilikataa kwa kuwa mfungaji alionekana kubahatisha.

IPP iliyokuwa inaundwa na mamluki watano, yaani wachezaji wasio waandishi wa habari iliweza kusawazisha katika dakika ya 67.

Mbali na timu hiyo ya IPP kuwa na usongo wa kusawazisha kwa kushambulia kwa nguvu, Twiga walitulia na kuonyesha kuwazidi mbinu za kimafunzo.

Timu hiyo ilipata bao la pili dakika ya 79 baada Asha Rashid aliyeng'ara katika mchezo huo kumtoka beki wa pembeni Jimmy Charles.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.