Msiogope Eto'o hatakuwepo-Kikwete
Rais Jakaya Kikwete amewataka wachezaji wa timu ya soka ya wanawake Twiga Stars kucheza kwa kujiamini, watakapopambana na timu ya Taifa ya wanawake ya Kameruni hapo kesho.
Kikwete aliyasema hayo kwa sababu Serikali inawajali pamoja na Watanzania wote, kwani timu hii ya Wanawake ya Twiga itapata moyo kwa kushangiliwa popote watakapokuwa.
Rais Kikwete alisema hayo juzi Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa chakula cha usiku alichowaandalia wachezaji wa Twiga Stars, ili kuwatia moyo na kuwafahamu kwa sababu walipokuwa kambini hakupata fursa ya kuwatembelea.
Rais aliweza kuwatakia kheri katika mechi ya kesho dhidi yao na Kameruni, aliwaeleza kwa kuwapa moyo kuwa, Kameruni ni jina kubwa katika soka la wanaume sio wanawake kwani hakutakuwepo na Eto'o na mtakapoingia kiwanjani hapo kesho muamini kwamba niko nanyi.
Aliwasihi kwamba wajiaminini na wafahamu kuwa ushindi ni wao na Watanzania wote wako nyuma yao, kwani Soka la wanawake halina muda mrefu kinachotakiwa ni kujiamini na kuungwa mkono.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa soka la wanawake Elizabeth Kalinga alimshukuru Rais kwa uamuzi wake wa busara wa kukutana na wachezaji hao na kusema kuwa, kitendo hicho ni cha uungwana na kimewaongezea vijana wake morali wa kushinda mpambano huo.
Naye Naibu Waziri Bendera jana aliweza kuwatembelea wachezaji hao kambini, na kuwataka wasiwaogope Kameruni kwani ina wachezaji kama wao.
Bendera alisema Twiga inatakiwa kucheza kwa kujiamini bila woga, wakiamini Watanzania wote wapo nyuma yao na wanategemea ushindi kutoka kwao.
Alimalizia kwa kusema kwamba Kameruni ni jina la nchi kama Tanzania na wachezaji wake hawana tofauti na wetu kama ni urefu huo ni kimo tu, kwani kinachotakiwa ni wachezaji kujituma kwa juhudi zao wakifata mafundisho ya walimu na hakika tutashinda mchezo huo.Bendera.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala