Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Tarehe ya mashindano yabadilika

Yale Mashindano ya mbio za baiskeli ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyopangwa kufanyika Jumapili ijayo yameahirishwa hadi hapo yatakapotangazwa tena baadaye mwaka huu.



Katibu kuu wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Dar es Salaam (CHABADA) Said Kengele, alisema kwamba wameamua kusogeza mbele mashindano hayo kutokana na kukosa udhamini.

Mashindano hayo yalipangwa kushirikisha jinsia zote mbili ambako, wanaume wangeshindana katika umbali wa km 150 na wanawake km 60.

Kengele alisema awali chama chake kiliomba udhamini kwa kampuni mbalimbali ili kufanikisha mashindano hayo, lakini mpaka kufikia jana hakukuwa na kampuni yoyote iliyokuwa imerudisha majibu ya maombi hayo.

Aliongeza kwa kusema kwamba CHABADA inahitaji sh milioni mbili kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo.

Alisema kuwa jumla ya wapanda baiskeli 30 wamethibitisha kushiriki mashindano hayo, na amewataka kuendelea kufanya mazoezi hadi watakapotangaziwa.

Mwaka jana chama hicho kiliandaa mashindano kama hayo katika mazingira magumu yaliyosababisha washindi kukabidhiwa mataji, ambao ni Abdeheman Hussein ambaye ndiye bingwa mtetezi, Allen Nyanginywa aliyeshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Michael Kasmeni.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.