JKT kuwanyamazisha wapinzani wao
Hatimaye Timu za JKT Wanaume kwa Wanawake ziling'ara katika mashindano ya mpira wa Kikapu 'Kili Super Cup' yaliyoanza kufanyika juzi ndani ya Uwanja wa Taifa hapa bongo.
Kwa upande wa wanawake JKT Stars ilianza vizuri baada ya kuwazamisha wapinzani wao wa jadi Jeshi Stars kwa pointi 64-46, ambapo hadi mapumziko washindi waliongoza kwa pointi 30-23.
Evodia Kazinja wa JKT Stars aliongoza kwa timu yake akifunga pointi 18, akifuatiwa na Esther Fanuel aliyefunga pointi 16, huku huku Grace Daudi 'Sister' wa Jeshi alifunga pointi 15 na Penina Kiwe alifunga 7.
Katika mchezo mwingine kwa wanaume JKT waliwafunga UDSM (Outsiders) kwa pointi 72-39, ambapo hadi mapumziko JKT walikuwa wanaongoza kwa pointi 31-13.
Ashraf Haroun wa JKT aliongoza kwa kupachika tena pointi 15 na Juma Kisoki alifunga 12, wakati wafungaji wa USDM aliyeongoza ni Claudio Kisanko aliyefunga pointi 11 na Ibrahimu Mwinyi alifunga pointi 9.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala