Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Twiga kuelekea mjini Younde Machi 6

Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake Twiga Stars inatarajia kutimka nchini Machi 6 kuelekea mjini Younde, Cameroon kwa ajili ya kwenda kuvaana na timu ya Wanawake ya Cameroon katika mechi ya maruadiano.



Mechi hiyo ya Marudiano kati ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania na timu ya Taifa ya Wanawake ya Cmeroon, imepangwa kupigwa kati ya Machi 7, 8 na 9.

Timu hizo zinawania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wanawake zilizopangwa kufanyika Equatorial Guinea mwishoni mwa mwaka huu.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Uwanja wa Taifa Twiga ilikubali kipigo cha mabao 3-0, hali inayoiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwani sasa itahitaji ushindi wa mabao 4-0.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Florian Kaijage alisema timu hiyo itaondoka licha ya kutoelezwa na wenyeji wao tarehe maalumu ya kuchezwa kwa mechi.

Kaijage alisema timu itaondoka Machi 6 kwa lengo la kufika mapema tayari kwa mchezo ambao unatarajia kufanyika kati ya Machi 7 hadi 9.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.