Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Ushindi ni wa kwetu-Julio

Hatimaye timu ya Watoto wa Msimbazi Simba ya timka jana nchini kuelekea Ethiopia, huku ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Awasa ya huko.



Mechi hiyo kati ya Simba na Awasa, inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii mjini humo.

Nahodha wa Klabu hiyo ya Simba Juma Kaseja alisema wanaenda kupambana na timu nzuri, na chochote kinaweza kutokea ila muhimu ni kushinda mechi hiyo.

Alisema Nahodha huyo kwamba wameshafanya maandalizi mazuri kulingana na timu wanayoenda kuvaana nayo, kwani ni timu nzuri chochote kinaweza kutokea ila muhimu ni kushinda mechi hiyo ili tuweze kusonga mbele katika michuano hii.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Simba Jamhuri Kihwelo, Julio alisema wanaenda kupambana ili kushinda mechi hiyo na kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa ya klabu Afrika.

Julio alisema wanaenda kumenyana na watu waliowabamiza mabao 3-0 hapa nyumbani, na isitoshe tunakwenda kucheza kwao ambako kuna baridi kwani tunaomba dua za Watanzania ili kushinda.

Kocha Mkuu wa Simba Milovan Cilkovic alisema wamejitayarisha vizuri kucheza mechi ya marudian, na Watanzania wajitayarishe kupokea matokeo mazuri.

Cilkovic alisema wamefanya maandalizi mazuri na wachezaji wote wakofiti katika mechi ya marudiano na Watanzania watarajie matokeo mazuri katika mechi ya marudiano dhidi ya Awasa.

Msafara huo ulioondoka jana ulikuwa wa watu 26 wachezaji 19 walioambatana na viongozi wao saba, na kiongozi wa msafara huo ni Muhsin Kosongo.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.