Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Gofu kutimua vumbi Jumamosi

Ile Michuano ya Gofu ya kuwania kombe la Nahodha (Captain Trophy), itatimua vumbi ndani ya viwanja vya Klabu ya Gymkhana kuanzia jumamosi hapa hapa jijini.



Michuano hiyo itakuwa ni ya siku mbili na inatarajia kushirikisha wachezaji katika makundi tofauti.

Makundi yatakayochuana siku kwenye michuano hiyo ya kila mwaka, ni wanaume daraja A, B, C, wanawake wakiwemo na vijana wadogo.

Michuano hiyo ya viwanja 36 ni maalumu kwa kumuaga nahodha anayemaliza muda wake, ambaye kwa sasa ni Dioniz Malinzi kabla ya kupisha uchaguzi mwingine utakaofanyika Machi 17 klabuni hapo.

Malinzi na kamati yake ya sasa akiwemo makamu David Mollel na katibu Adam Ngamilo waliochaguliwa mwaka jana wanamaliza muda wao ingawa wana nafasi ya kuchaguliwa tena.

Washindi watakao patikana ndani ya michuano hiyo wanatarajia kukabidhiwa zawadi katika hafla itakayofanyika klabuni hapo Jumapili mara baada ya michuano.

Hata hivyo mchezaji bora wa gofu mwaka 2007 ni chipukizi Geoffrey Leveriana na Hassan Kadio, watakosa michuano ya mwaka huu kutokana na kuwa safarini Afrika Kusini.

Wachezaji wao watakuwa Afrika Kusini kushiriki michuano ya Kimataifa ya Wazi ya Ridhaa ya Sanlam, iliyopangwa kuanza Machi 3 hadi 7 kwenye viwanja vya Royal Durban nchini humo.








 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.