safari hii sitaki utani-Maximo
Hatimaye Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Marcio Maximo, asema anatarajia kuita kikosi kipya chenye wachezaji 26 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajia kufanyika Machi 26.
Kocha huyo alisema kikosi hicho kinatarajia kutangazwa Machi 14, kikiwa na sura mpya wakiwemo wachezaji chipukizi aliovuna wakati wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaoendelea.
Kikosi hicho kitaingia kambini Machi 22 na kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo, ili kujiandaa na michezo yake ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2010.
Alisema anatarajia kuita kikosi kingine kwani wengi wa wachezaji ni wapya, na wengi wao hawajawahi kuingia katika timu lakini kutokana na viwango vyao wanavyoonesha katika ligi nimewakubali kuwa wananifaa katika timu yangu.
Maximo alisema hiyo ndiyo hali halisi ya timu hiyo, ambapo kila wakati analazimika kuita wachezaji wapya ambao viwango vyao vimeonekana kuwa juu.
Alisema mbali ya kuita wachezaji wapya katika kikosi hicho bado ataendelea kuwaita wachezaji mbalimbali, waliopitia katika timu hiyo ambao wameendelea kuboresha viwango vyao.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala