Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Sina mpinzani ndani ya familia ya Matumla

Bondia Francis Cheka aliwezakutisha kwamba hana mpinzani katika familia ya Matumla, baada ya kumchakaza kwa Knockout (KO) katika raundi ya 10 katika pambano la raundi 12.



Bondia huyo aliweza kufanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kumkung'uta mpinzani wake, kwani aliwahi tena kushimnda mara mbili kaka wa Hassan mkongwe Rashid Matumla 'Snake Boy' bungwa wa zamani wa dunia wa WBU na IBU.

Pambano hilo lilichezwa juzi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hapa hapa nyumbani, Cheka maarufu kama 'SMG' alimwangusha Matumla katika raundi ya 10 kwa makonde ya mfululizo kabla ya kummalizia kwa konde kali la kushoto lililomfanya aanguke kama 'kifurushi cha gunia'.

Katika pambano hilo la raundi 12, Matumla maarufu kama Red Bull alizidiwa, na ndipo bondia Cheka aliweza kuwapa matumaini mashabiki wake kwa ngumi za kushitukiza.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.