Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
10 waenda Kenya

Wachezaji wapatao 10 wa mchezo wa gofu ya ridhaa kutoka Klabu ya Gymkhana jijini, walitimka jana kwa basi kuelekea Nairobi, Kenya, kushiriki michuano ya Pro-Am Kenya Open iliyopangwa kufanyika kwenye Klabu ya Karen, Nairobi hapo kesho kutwa.



Wachezaji hao wataungana na wachezaji wawili wa kulipwa Adam Mohamed na Fadhil Nkya ambao pia watashiriki michuano ya siku nne ya Kenya Open iliyopangwa kuanza baada ya Pro-Am kwenye viwanja hivyo.

Wachezaji hao wanatarajia kuondoka leo kwa ndege kuelekea Nairobi tayari kwa michuano hiyo.

Kati ya wachezaji hao 10 wa ridhaa, wanne ni wanawake ambao wamepewa nafasi ya kushiriki Pro-Am michuano ambayo inashirikisha wachezaji wa kulipwa na wa ridhaa wanaume.

Wachezaji walioondoka ni Mchezaji Bora wa gofu Tanzania mwaka 2007, Geoffrey Leverian, Hassan Kadio, Iddi Mzaki, Bryceson Nyenza, Athumani Chiundu na Pembe Kondo.

Wachezaji wanawake walioondoka ni chipukizi Angel Eaton, Ayne Magombe, Hawa Wanyeche na Shazi Myombe.

Mwaka jana mchezaji mwandamizi mhazili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mohabe Nyirabu aliibuka mshindi wa taji la Pro-Am akishirikiana na Dickson Katibi wa Kenya ambao kila mmoja alipata mikwaju neti 63 na mchezaji wa kulipwa kutoka Scotland, Graeme Brown aliyepiga mikwaju gross 64.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.