Cheka atikisa Morogoro
Bondia Francis Cheka kutoka Morogoro 'mji kasoro bahari' alipokelewa kwa mbwembwe zote, baada ya kumshinda mpinzani wake Hassan Matumla.
Mmasumbwi huyo aliweza kuwarudisha mashabiki wengi wa mchezo huo wa ngumi mkoani Morogoro ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali.
Cheka aliwezakukanyaga ardhi ya mkoa huo akiwa ndani ya gari la wazi majira ya saa 5:30 asubuhi, huku watu ukijipanga pembezoni mwa barabara kwa kumlaki.
Pia mapokezi hayo yaliweza kuongozwa na Mkuu wa wilaya wa Morogoro Sjini,Said Mwambungu, aliyeambatana na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Dr. Omari Mzeru pamoja na Mjumbe wa Halmsahauri Kuu ya CCM Aziz Abood akiwemo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Thobias Andengenye.
Cheka aliwapongeza wakazi wa Morogoro katika ukumbi wa Manispaa, kutokana na ushirikiano wao uliochangia aibuke na ushindi dhidi ya Matumla.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro alisema kitendo cha Cheka kutwaa ubingwa, kumezidi kuiongezea sifa Morogoro na kiasi cha sh. milioni 2 kilichangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kumpongeza bondia huyo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala