Elimu na Michezo havitenganishwi-Bendera
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Joel Nkaya Bender, aliweza kuipongeza Taasisi ya Tanzania Sports Academy (TSA) ya Ilboru kwa kuwa juu katika kiwango cha Michezo ya Winning Sport.
Bendera aliweza kutoa pongezi hizo wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi, na katika shule hiyo inayotarajiwa kujengwa ndani ya kijiji cha Mkonoo Kata ya Terrat, Manispaa ya Arusha.
Alisema ujenzi wa shule hiyo ambayo ni ya pekee na ya kwanza hapa nchini, ni jambo la kuigwa na kupongezwa kwani ni chachu ya mafanikio katika maendeleo ya michezo Tanzania.
Naibu huyo alisema suala la elimu na michezo ni mambo ambayo hayawezi kutenganishwa, kwani mwanamichezo aliyesoma ana uwezo mkubwa wa kushika na kuheshimu maadili ya michezo.
Alisema anapenda kumpongeza Mkurugenzi wa TSA Maximilian Iranqhe, kwa kuanzisha kitu hiki, kwani pole pole ndiyo mwendo na mkoa huo una hazina kubwa ya vipaji vya wanariadha hasa wa mbio ndefu.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala