Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Chang'ombe Boys yafutwa klabu bingwa

Ile Timu ya mpira wa kikapu ya Chang'ombe Boys yafutwa kushiriki mashindano ya Klabu bingwa Taifa (NBL), yatakayoanza Marchi 25 jijini Tanga.



Timu hiyo iliweza kufungiwa na chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BD), kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Iliweza kupewa barua ya ushiriki na Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania (TBF), ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo lakini BD waliwapiga chini kutokushiriki mashindano hayo kwa sababu ya kufungiawa.

Mkurugenzi mtendaji wa BD Mbaga Mwamboma alisema bado hawajakaa kikao tena kuijadili timu hiyo, licha ya kutoa adhabu hiyo ya awali lakini ushiriki wa Chang'ombe kwenye mashindano ya taifa ulikuwa mikononi mwa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF).

Naye Katibu mkuu wa TBF Lawrence Cheyo alisema ni kweli waliweza kupokea barua hiyo kutoka BD, na wamekwisha ijadili na wametoa maamuzi.

Na ndo maana timu ya Chang'ombe Boys imefutwa kwenye NBL
kwa sababu imefungiwa kutokana na kutokuwa na utovu wa nidhamu, na TBF hawawezi wakaleta timu ambazo hazina nidhamu watulie na waangalie tatizo liko wapi.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.