Twiga Stars wakabidhiwa Bendera
Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars waliweza kukabidhiwa Bendera jana na kuweza kutimua hapa kwa ndege ya Kenya Aiways, kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika mjini Younde,Cameroon Jumamosi.
Naibuu waziri wa Michezo Joel Bendera aliweza kukabidhi Bendera hiyo kwa kiongozi wa msafara huo Elizabeth Kalinga, na aliwaeleza wachezaji hao kuwa watanzania wanaimani kubwa nawao watarejea na ushindi.
Aliweza kukabidhi bendera hiyo ikiwa ni alama ya kuonyesha kuwa wachezaji hao hawako peke yao huko Cameroon, bali watanzania wapo pamoja nao.
Alisema kwamba kufanya vibaya katika mchezo uliopita si kikwazo cha wao kushindwa kufanya vizuri, bali ni matokeo katika mchezo na vilevile wakumbuke kuna mambo matatu kufungwa, kutoka sare na kushinda.
Aliwasisitiza wachezaji hao kuwa kikubwa wanachotakiwa kufahamu, ni pamoja na kujifunza nidhamu kwa viongozi wao ili waweze kufanikiwa zaidi.
Naye nahodha wa timu hiyo alitoa shukrani zake kwa wadau wote waliofanikisha safari yao, na kuwaahidi watanzania kuwa wakoteyari kurudi na ushindi nyumbani kwani wanajiamini kwa yale waliyofanya kwenye mazoezi.
Wachezaji walioondoka ni Fatuma Omari,Fatuma Bushiri,Pulkaria Chalagi,Etoo Mlezi,Tina Victor,Mwanahidi Abdalah, Neema Munishi, Asha Rashidi, Sophia Mwasikili, Mwanahamisi Omary, Ester Chabruma, Fatuma Hatibu, Mwapewa Mtumwa, Mwanahamisi Omary, Helen Peter, Mwanahidi Yusuph na Mary Masatu.
Kwa upande wa viongozi ni Elizabeth Kalinga, Furaha Fransis, Boniface Mkwasa, Sufiani juma na Mohamed Richad.
Ila wachezaji saba wameachwa kutokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili, likiwemo kuumwa na wengine kukosa ya tiketi.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala