Waliovunja nyumba Dar kutemwa mzigoni
Serikali Mkoani Dar es Salaam imeagiza Mhandisi na Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, wafukuzwe kazi kwa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kusimamia ubomoaji za nyumba za baadhi ya wakazi wa Tabata Dampo.
RC wa Dar Abbas Kandoro asema jijini Dar es salaam kuwa
adhabu hiyo pia itamhusishe, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Lubuva endapo atabainika kuhusika moja kwa moja ama kwa kuamuru kufanyika au kubariki ubomoaji wa nyumba hizo.
" Nimeagiza watendaji wote wa Manispaa ya Ilala waliohusika katika zoezi hilo wafukuzwe kazi hasa Mhandisi, Mwanasheria na hata Mkurugenzi akibainika alishiriki moja kwa moja," alisema Kandoro.
Akielezea sababu za hatua hiyo kali kwa watendaji hao, Kandoro alisema imetokana na ama uzembe au kutowajibika kwao katika maamuzi yao, hivyo kusababisha uvunjaji wa haki za wakazi wa eneo hilo kutokana na nyumba zao kuvunjwa Februari 29, mwaka huu.
Alisema kitendo cha uongozi wa manispaa hiyo, kuwabomolea
nyumba wakazi hao, siyo cha kiungwana na kimekiuka misingi ya haki za binadamu na utawala bora, taratibu na sheria.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala