Barua ya Bush kwa WATZ.
Rais George W. Bush wa Marekani, ameahidi kuendelea kufanya kazi na Rais JK pamoja na viongozi wengine, ili kuisaidia Bongo kushughulikia changamoto zinazoikabili.
Katika barua yake kwa Rais JK Kikwete na Watanzania wote iliyotolewa na ofisi ya ubalozi wa Marekani nchini, Bw. Bush alisema serikali yake itaendelea kuipiga bongo tafu.
``Tunashukuru kwa urafiki wake na urafiki wenu, tutaendelea kutoa misaada yetu wakati mnapozidi kusonga mbele,`` ilisema sehemu ya barua hiyo.
Bw. Bush ameandika barua hiyo akitoa shukrani kwa Watanzania kufuatia ziara ya siku nne aliyoifanya mwezi uliopita nchini pamoja na mkewe Bi. Laura na akaahidi kutembelea tena nchini miaka ijayo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala