Maisha ya jela yamfanya akate uume .
Mkazi wa Kijiji cha Sazira, wilayani Bunda Mkoa wa Mara, anayeshitakiwa kwa tuhuma za kuua watu watatu wa familia moja, akiwemo mke wake, amejikata sehemu zake za siri akiwa ndani ya chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Bunda,
wakati mahakama ikiendelea na vikao vyake.
Mtuhumiwa huyo, Pande John (35), mkazi wa mkoani Shinyanga, aliyekuwa akiishi mkoani Mara, alijikata sehemu zake za siri kwa kutumia wembe aliokuwa nao.
Kutokana na kitendo hicho, ilibidi shughuli za mahakama hiyo zisimame kwa muda na polisi kulazimika kumkimbiza majeruhi huyo hospitalini kwa matibabu zaidi.
Imeelezwa kuwa, mtuhumiwa huyo alitibiwa akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, ambako madaktari walisema alijikata na kukaribia na mrija wa uume wake.
Mwedesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Edward Manoni, alisema mtuhumiwa huyo alijikata sehemu zake za siri, akiwa kwenye chumba cha mahabusu na kwamba alivuja damu nyingi na kuwachafua mahabusu waliokuwa jirani yake.
Kwa mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Richard Maganga, mtuhumiwa huyo anashitakiwa kwa tuhuma za mauaji ya watu watatu wa familia moja, akiwemo mke wake, baba na mama mkwe wake, aliowavamia nyumbani kwao usiku, wakiwa wamelela.
Aidha, jeshi la polisi lilisema kuwa baada ya kumhoji mtuhumiwa huyo, imebainika kuwa kilichosababisha achukue uamuzi huo ni kushindwa kuishi maisha ya gerezani, hivyo ni vema afariki dunia ili kuepukana na kero hiyo.
Inspekita Manoni alisema, mtuhumiwa huyo atafunguliwa kesi nyingine ya kujaribu kujiua kwa kutumia wembe na kujijeruhi vibaya.
Kesi ya mtuhumiwa huyo ya kuua watu watatu wa famila moja imehairishwa hadi Machi 13, mwaka huu, itakapotajwa tena mahakamani hapo kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala