Usajili watahiniwa mtandaoni.
SERIKALI imezindua mfumo mpya wa usajili wa watahiniwa wa kujitegemea na wa shule za msingi na sekondari nchini kwa njia ya mtandao wa intaneti.
Mfumo huo ulioandaliwa na Baraza La Mitihani la Taifa (NECTA) kwa kushirikiana na Wataalamu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, utatumiwa nchini nzima kusajili wanafunzi shuleni.
Akizindua mfumo huo kwenye Mkutano Mkuu wa Pili wa Elimu, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe alisema kuwa, utarahisisha usajili wa watahiniwa nchini kote, hivyo kuleta ufanisi.
Alisema alifafanua kuwa ili kuhakikisha azma hiyo inatimia, maeneo yasiyo na umeme yatapelekewa umeme unaotumia nishati ya jua na kuwaagiza wamiliki wa shule binafsi, kujiandaa kwa hilo.
" Hakutakuwa na visingizio, tutatumia mfumo huu katika kusajili watoto kuanzia mwaka ujao, hata private wafanye juhudi kuweka vifaa kuwezesha hilo, alisisitiza Profesa Maghembe.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako, alisema hayo ni matunda ya ubunifu wa wataalam wa mifumo ya kompyuta wa baraza na wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala