Gonjwa la kulia na kukimbia laja.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, umeibuka ugonjwa wa ajabu wa kulia na kukimbia ovyo katika mkoa wa Mwanza.
Wanafuzi wa Shule ya Sekondari ya Chigunga iliyoko katika kata ya Chigunga Tarafa ya Butundwe wilayani Geita mkoani Mwanza, wamekumbwa na ugonjwa wa ajabu.
wanafunzi 20 wa kike na wa kiume saba wamekumbwa na ugonjwa huo unaosababisha kupoteza fahamu pindi wanapokumbwa na hali hiyo.
Makamu Mkuu wa shule hiyo, Peter Machege, alisema hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa walimu na wanafunzi.
Alisema kwa sasa hali ni mbaya zaidi kwani ugonjwa huo huwakumba kati ya wanafunzi watano hadi 10 kwa siku moja, tofauti na wakati ulipoanza, kwa kuwakumba wanafunzi wawili hadi wanne .
“Lakini kilichotuchanganya zaidi ni kwamba ugonjwa huu umehamia hadi kwa wavulana ambao awali hawakuwa na hali hiyo, hali ni mbaya hasa wanapokumbwa na hali hiyo wanakuwa na nguvu za ajabu na kuwapiga wenzao darasani,” alisema makamu mkuu wa shule, na kuongeza kuwa hali hiyo inawakumba wanafunzi wa kidato cha pili na
tatu pekee.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala