Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
TASWA yamchagua Amour wa Judo

Hati maye Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) wiki iliyopita, kiliweza kumchagua mchezaji wa Judo Masoud Amour kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari.



Naye Mwenyekiti wa TASWA Boniface Wambura alisema Amour aliweza kupata kura 101, na hivyo kuweza kumpiku Faraja Mlaki pamoja na Semeni Mlanzi.

Wambura alisema Amour alitwaa ubingwa huo katika mashindano kutokana na sifa alizokuwa nazo, ikiwemo kuwa bingwa wa Judo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Na alitwaa ubingwa huo katika mashindano yaliyofanyika Burundi na kuweza kujitwalia Medali ya Dhahabu.

Kura alizopigiwa Mlaki ambaye ni mchezaji wa mpira wa pete alipata kura 76, huku mwenzake Mlanzi ambaye ni mchezaji wa mpira wa mikono alijitwalia kura 72.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.