Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Ufisadi BOT ngoma nzito.

Timu ya Rais kuchunguza watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu Tanzania (BoT), imekiri kuwa kazi ya kuyakamata mafisadi ni ngumu kwani hadi sasa imefanikiwa kuyajua makampuni yaliyohusika tu.

Badala yake, timu hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG), Johnson Mwanyika imejitetea kwamba, hadi sasa uchunguzi wao umebaini wahusika wakuu ni makampuni ambayo ni tofauti na watu.

Hata hivyo, kauli hiyo mpya ya Mwanyika imeshindwa kujibu hoja ya msingi ya wanaharakati ambayo imezingatia kauli ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo, ambaye alisema serikali imeshapokea Sh50 bilioni za EPA lakini akasita kutaja majina ya watuhumiwa.

"Kumekuwa na malalamiko ya kutokamatwa kwa waliohusika.
Tunapenda kuueleza umma kwamba, uchunguzi wetu hadi
hivi sasa unaonyesha kwamba wahusika wakuu ni
makampuni. Kisheria, makampuni hayo ni mtu yaani
Legal Person," alisema Mwanyika na kuongeza:

Mwanyika alisema uchunguzi huo unaendelea na ndiyo
utakaowezesha kujua hatua za kisheria zitakazochukuliwa, alisisitiza katika taarifa yake baada ya kikao cha dharura kuhusu mchakato huo.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.