Wauaji wanywa damu ya albino.
Serikali mkoani Mwanza, imesema inasikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu vya kuwachinja albino, kunywa damu na kutoweka na viungo vyao.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk James
Msekela, wakati wa madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Dk Msekela, alisema kitendo cha baadhi ya watu kuamua kuwachinja wenzao kama kuku, kunywa damu yao na kutoweka na baadhi ya viungo, kimemsikitisha kwa kuwa ni cha kinyama na kisichokuwa na chembe ya utu hata kidogo.
" Kuna tukio la mauaji ya albino lilitokea huko wilayani Kwimba , wauaji waliamua kumchinja albino, kukinga damu kisha kunywa na baadaye kumtenganisha miguu na mapaja na kutoweka na miguu," alisema
Alisema tukio hilo binafsi lilimsikitisha kwa kuwa mauaji hayo ya kinyama yalifanyika wakati mabinti wawili wakiwa wamelala na albino huyo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala